Utambulisho na msingi wa huduma
PROPHETIC INTERNATIONAL OMEGA CHURCH (PIOM CHURCH)
Historia, maono, kusudi, misingi ya imani, wito maalumu, historia ya mwanzilishi na maadili ya huduma.
1. HISTORIA YA HUDUMA YA PROPHETIC INTERNATIONAL OMEGA CHURCH ( PIOM CHURCH )
Huduma hii ni wito wa MUNGU alio nipatia kwa kusudi la kuwafikia wake alio wakusudia kwasababu Kila wakati Mungu anapo taka kufanya jambo huwa ana inua mtu MMOJA ili amtumie kwa niaba yake sawa na MATHAYO 22:14 Hivyo huduma hii ilianza na mtu MMOJA ambae ni kiongozi wa huduma ( mbeba maono ) Prophet Daniel Moshi kama Mchungaji kiongozi wa huduma hii baada ya kusimama mim katika wito huu ndipo Mungu alipo nikutanisha na washrika wengine 2 mke na mume ambao walikuwa ni watu Muhimu sana kwenye MAONO ya huduma hii kwasababu wakati ambao Mungu ana niita na kunipa kusudi hili au kazi hii sikuwa na chochote , sikuwa na ardhi MAHALI pa kufanyia ibada ,hivyo WALIPO kuja watu Hawa waliniwezesha sana kunipatia ardhi kwaajili ya huduma na ndipo huduma ya Piom ilipo anza Mwaka 2015 Iliyo anzia Jijini Dar es salaam wilaya bagamoyo Kata ya Mbwen MTAA wa Mikochen huduma ilia anza na watu watatu yaani Mimi , na washrika wafamilia Moja yani mke na mume ndipo Mungu alipo anza kuwaleta watu na ndipo tulipo anza kuongezeka na kuzidi kwa kadri siku zilivyo kwenda
Mwaka 2017 tulipata neema zaidi ya kuhama kutoka Mbwen Mikochen Wilaya ya Bagamoyo mpaka Mbwen Masaiti wilaya ya Kinondoni MTAA wa Masaiti ambapo tulifanya huduma pale kwa mafanikio makubwa ya kiroho watu wakimpokea Yesu , kukuwa kiroho na KUTEMBEA katika UWEPO wa Mungu mpaka Mwaka 2022 tupo pata neema tena ya kuhama kama ilivyo HISTORIA ya KANISA la Kwenye biblia LILILO ongozwa na Musa utaona lilikuwa Lina tembea kuelekea kanaani safari hiyo tuna ifananisha na sisi kwamba tulikuwa tuna hama kuelekea kanaani yetu ya kanisa
Hivyo Mwaka 2022 tukahamia Tegeta Wilaya ya Kinondoni mtaa wa Makamba katika Ukumbi wa Bonden Park ambapo tupo mpaka hivi sasa 2026 tukiendesha ibada ZETU na Mungu ame kuwa ni mwaminifu sana kwa kudhihirisha Nguvu,Uwezo na Neema inayo inatenda mambo makubwa na ya AJABU Sana sawa na WAEFESO 3:20
2. MAONO YA KANISA
Maono ya kanisa la Piom ni kuwafikia watu wengi zaidi mpaka Ulimwengu wote sawa na neno la Mungu MARKO 16:15
Tuna MAONO ya kuifikia Dunia kwa neno la Mungu lisilo ghoshiwa ( kuchanganywa ) na ufanganyifu wowote ule 1PETRO 2:2 ili liweze KUSABABISHA mabadiriko kwa watakao liamini na kulipokea , mabadiriko ya kitabia,kiafya,kiroho,hata kimaisha kwasababu neno la Mungu limebeba uwezo wa kugeuza hivyo linapo kuja kwenye maisha ya mtu lazima litamgeuza , kama liliweza kugeuza maji kuwa Divai halishindwi kumgeuza mwizi akawa MUHUBIRI wa Injili , Kahaba akawa Mke wa mume mmoja na Masikini akawa Tajiri .
Pia kanisa letu ni la KINABII , linalo tembea katika MAONO ya Kinabii lakini pamoja na yote tuna amini katika huduma zote 5 za Roho sawa 1WAKORINTHO 12:8-10 Hivyo tuna tambua UWEPO na umuhimu wa Mitume,Wachungaji,Waalimu, Wainjilisti na Manabii wote ni watumishi wa Mungu na tuna shirikiana na kuungana Mkono katika kulitumikia kusudi la MUNGU
Lakini pia tuna MAONO sisi kama kanisa la Piom kuhakikisha watu Wana MWAMINI Yesu na KUPOKEA kuwa Bwana na mwokozi wa maisha Yao kama ilivyo andikwa YOHANA 1:11-12 Bali wote walio mpokea aliwapa uwezo wa kufanyika Wana wa Mungu
Hivyo tuna tamani watu wote wageuzwe na kuwa Wana wa Mungu kwa KUPOKEA Yesu Kristo awe bwana na mwokozi wa maisha Yao
Malengo ya kuwafikia watu wengi
Kwa neema ya Mungu tuna MWAMINI Mungu katika kuhubiri kupitia huduma hizi Muhimu
(1) Television Tv
Tuna amini kwamba kwa neema ya Mungu tuta kwenda katika media mbali mbali au Tv mbali mbali ili kulifikisha neno la Mungu kwa Kila kiumbe sawa na MARKO 16:15
(2) OUTREACH SERVICES / HUDUMA ZA NJE YA KANISA
Tuna Mipango mikubwa ya kuwa na Mikutano ya nje ya kanisa letu kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi ili walisikie neno la Mungu lilibeba Uzima na Jawabu la maswali Yao , Kuna watu Wana maswali kuhusu Afya zao,NDOA zao,Familia yako ,Elimu zao na Bado hawaja patiwa MAJIBU na mwenye majibu Yao ni Yesu Pekee na Yesu ni neno la Mungu sawa YOHANA 1:1-5 Hivyo mtu anapo lisikia neno na kulipokea anapokea MAJIBU ya maswali yake.
(3)Mwisho tuta kuwa na huduma za Uinjilisti mitaani
Hii ni huduma ya kutoka nje kwenda barabaran na mitaani na kuongea na watu kwa kuwahubiri habari za Yesu,kuwapa vipeperushi vyenye neno la Mungu na Muongozo wa maombi ya Toba, lakini vitakavyo wanesha umuhimu wa kufika katika kanisa na kuwalekeza Jinsi watakavyo weza kufika kanisan
3. KUSUDI LA HUDUMA / KANISA
Kusudi la huduma hii ni kutuweka tayal au kutuandaa kwaajili ya ujio wa Yesu Kristo kama neno linavyo sema 2 Timotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
Neno linataka tuwe tayal muda wote na sababu za kuwa tayal ni kwasababu Yesu alisema kuwa hakuna anae jua siku Wala saa ambayo mwana wa adamu atakapo Rudi kulinyakuwa kanisa lake hivyo kanisa ni MAHALI pa maandalizi hata siku Yesu akasema ana Rudi ghafra ana wakuta watu walio tayal kuondoka nae MATHAYO 24:36 na MARKO 13:32
Ndio maana kanisa la Piom lina wafanya watu waishi maisha ya UTAKATIFU ambao katika huo hakuna mtu Alie muona Muona Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
4. MISINGI YA IMANI
Kanisa letu lina misingi mingi ya Imani lakini kubwa kuliko yote ni hili
(a)YESU NI MUNGU
Kanisa letu au KANISANI KWETU tuna amini Yesu ni Mungu bila kuwa na wasiwasi Wala mashaka yeyote ili kwasababu za msingi zinazo onekana katika bilia
Maandiko kadha wa kadha Yana onesha Ukweli wa jambo hili kuwa Yesu ni mwana wa Mungu tukianza na neno hili
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Mwana wa Mungu
Ana sema Mungu alimtoa mwanae wa Pekee kama Yesu ni mtoto wa Mungu basi Yesu ni Mungu kwasababu kitu chochote kinacho ZAA huzaa kinacho fanana na chenyewe mfano mtu huzaa mtu , Ng'ombe huzaa Ng'ombe na kondoo huzaa Kondoo basi kama Mungu anasema ni mwanae maana yake alizaa kwa namna ya kiroho tusiyo ijua sisi kwamaana hiyo Yesu ni Mungu kwa asilimia mia Moja
Ukweli mkubwa ni huu hapa ya kwamba Yesu ni Mungu mwenyewe soma maandiko haya ambayo Yesu alikuwa akimjibu Filipo yatosha kusema Yesu ni Mungu
Yohana 14:8-9
8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
(b) Utajiri ni Haki yetu na ni mapenzi ya Mungu tutajirike .
Utajiri ni taswira ya Mungu mwenyewe, sawa na maandiko haya Hagai 2:8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.
Kama Fedha na dhahabu ni mali ya Bwana na sisi ni watoto wake na kawaida watoto huziishi mali za wazazi wao Ina maana Mali na Utajiri wa Mungu ni WA kwetu , hivyo tuna amini kabisa kuwa Tajiri ni kuibeba sura ya Mungu kwasababu yeye sio masikini hivyo Kila Alie fanyika mwanae ana takiwa afanane nae katika Kila kitu soma hapa Tena Kumbukumbu la Torati 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Mungu ana jali sana Kiasi kwamba ana tupatia NGUVU zake zitakazo weza kutupekeka kwenye Utajiri na mafanikio kumbe hata mapenzi ya Mungu ni kwamba tufanikiwe katika mambo yote hasa Uchumi na maendeleo 3 Yohana 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Mungu ana taka tufanikiwe ndio maana sisi kama Wana Piom tuna amini katika MAFANIKIO ya Kiroho, Kiuchumi, Kijamii na kimaendeleo
5. WITO MAALUMU
Mungu anapo taka kuongea na mtu au watu au anapo taka kuwafikia watu , Taifa , au Jamii humuita mtu MMOJA au humchagua mtu MMOJA atakae simama kwa Niaba yake ili aka muwakilishe kwa mtu au watu nchi au Jamii,
Wakati wowote unamuona Waziri mkuu au Makamu wa Raisi yupo pale kwa kumuwakilisha kiongozi wake Raisi kwahiyo Haina tofauti na mtumishi wa Mungu unapo muona ana ongea au ana hudumu yupo pale kwa Niaba ya kiongozi wake Yesu Kristo,
Kiongozi wa kanisa la Piom ( Prophet Daniel Moshi ) ame itwa na Mungu ili amtumikie Mungu kwa kusudi la kufikisha UJUMBE kwa wale ambao Mungu ame wakusudia , kanisa la Piom ni kanisa ambalo Mungu ame likusudia na kulianzisha mwenyewe ndio maana hatujawa na misaada yeyote kutokea nje tangu tume anza , hatuja na harambee yeyote tangu tume anza hatujawa na makongamano ya changizo tangu tume anza lakini Mungu mwenyewe ame kuwa mwaminifu akitusimamia HATUA kwa HATUA tukivuka na kuendelea kusogea kwenye HATUA Mpya na za UTUKUFU
6. HISTORIA FUPI YA PROPHET DANIEL MOSHI
Prophet Daniel Moshi ni MUHUBIRI wa Injili ya Yesu Kristo alie itwa na Mungu kuwa Nabii kiongozi na mbeba MAONO ya Kanisa la PIOM Lenye maana Prophetic international Omega Church lenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam Tanzania
Prophet Daniel Moshi alipokea neema hii ya WOKOVU miaka mingi iliyo pita katika kanisa la GCTC Maarufu kama KANISA LA UFUFUO NA UZIMA lililo chini ya Kiongozi na mbeba MAONO ASKOFU DR.JOSEPHAT MATHIAS GWAJIMA ambae ndie Alie niongoza Sala ya Toba kutokea katika Dini ya Kiislamu
Ndipo safari ya maisha yangu na Kristo ilipo anzia mpaka hivi Leo nime somea mafunzo ya uchungaji kanisa hapo UFUFUO na Uzima Nina mpenda Askofu Dr Josephat GWAJIMA kwasababu ndio mlezi na MZAZI wangu wa KIROHO Mungu amtunze sana baada ya hapo ndipo nilipo itwa na kuchaguliwa na Mungu mwenyewe na KUPEWA wito huu ninao utumikia leo hii ndani ya kanisa la Piom Church
7. MAADIRI NA MISINGI YA HUDUMA
Maadili yetu yanatokana na neno la Mungu,kile ambacho neno lina ruhusu tuta fanya na kile ambacho neno haliruhudu basi hicho kwetu hatuta fanya
Mfano :
Swala la Mavazi sisi tunayo maadili yetu ya uvaaji katika kanisa letu Moja ya maadili yetu ni kwamba tuna vaa ili kujisitiri na sio kupendeza Japo kuwa tuna pendeza tunapo vaa lakini kusudi mama la kuvaa ni kujisitiri ( Kuficha uchi ) kupendeza Kuna fuata BAADAE
Kwasababu hata anae vaa uchi anapendeza pia lakini ana kuwa ame vunja kusudi mama la kuvaa nguo hii inatokana na namna Mungu alivyo mshonea nguo za miti Adamu na Eva Mwanzo 3:21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Sababu za Mungu kuwashonea nguo Adamu na Eva ilikuwa ni Kuficha uji wao ambao ulikuwa wazi kwasababu ya DHAMBI , hapo ndipo tunapo jifunza kuwa kumbe kusudi la kuvaa nguo ni Kuficha uchi lenye maana ya kujisitiri hivo kanisa letu linazingatia maadili haya Muhimu SANA ili kufanya kanisa likae katika misingi na UWEPO wa Mungu USIO weza kuondolewa na baadhi ya MILANGO ITAKAYO leta au KUSABABISHA watu kuingia katika mitego ya majaribu ITAKAYO sababisha anguko la watu katika dhambi
Biblia Ina sema ikimbieni zinaa , huku Mavazi yanaweza kuchangia Zinaa kusambaa kwa asilimia kubwa ndio maana utaona Makahaba Wana Mavazi yao ili wapate wateja kumbe Kuna Mavazi yapo kimkakati kabisa ili kuwanasa watu katika mtego wa zinaa hayo Mavazi yakiingia kanisa tayali kanisa lina kamatwa na Roho ya uzinzi na zinaa biblia Ina sema 1 Wakorintho 6:18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Hauwezi kuikimbia Zinaa kama USIPO shugurika na HATUA za mwanzoni hasa katika Mavazi , mipaka ya Kijinsia na Baada ya TABIA ambazo Zina weza sababisha zinaa ikachukua NAFASI
Kwahiyo sisi Wana Piom hatuvai ili tupendeze kwanza tuna anza na kusudi la kuvaa ili kujisitiri ( Kuficha Uchi ) harafu itafuata kupendeza BAADAE
Mwisho kabisa tuna heshimu mipaka ya Kijinsia , tukisema msemo huu " Tofauti zetu ni bayana " wakike ni WA kike na WA kiume ni WA kiume lazima kuwe na mipaka inayo oneka utofauti WETU lakini pia lazima tuwe na Heshima inayo inayo tufanya KUONA kuwa hatupaswi kusogeleana kwenye Viwango vya kugusana baadhi ya maeneo ya miili hasa pale inapokuwa si mke wako Wala mume wako kwasababu zinaa haikimbiwi kwa maombi bali kwa kujiepusha na mazingira YANAYO weza KUSABABISHA ukaanguka katika Zinaa
Yusuph alikimbia akaacha nguo ili asinguke katika Zinaa , hatupaswi kuleta utani kwenye swala la zinaa na Mungu atusaidie na akusaidie na wew pia sema Amen